Fri, 03 Oct 2025 | 09:44 AM
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mha.Dkt. Prosper Mgaya, amezindua rasmi Bonanza la Michezo la Wafanyakazi kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa NIT.
Bonanza hilo limefanyika Septemba 22, 2025, katika viwanja vya Chuo vilivyopo Mabibo jijini Dar es Salaam likihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa kikapu, kuvuta kamba, kufukuza kuku na mazoezi ya viungo vya mwili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Mgaya alieleza kuwa lengo la bonanza hilo ni kuimarisha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi, pamoja na kuchangia katika kuboresha afya na ustawi wa wanajumuiya wa NIT.
“Lengo letu ni kuongeza ari ya utendaji kazi kupitia michezo, afya njema na mshikamano baina ya watumishi na jamii ya Chuo kwa ujumla,” alisema Dkt. Mgaya.
Aidha, Dkt. Mgaya aliahidi kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Maandalizi ya bonanza hilo, hususa ni kuhusu ukarabati wa miundombinu ya michezo Chuoni .
Bonanza hili ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya mafanikio ya Chuo katika kutoa mafunzo mbalimbali katika sekta ya usafirishaji.
50 YEARS NIT ANNIVERSARY 1975-2025
"Excellence in Transport for Sustainable Economy"