National Institute of Transport - NIT
Bonyeza Kuthibitisha

LATEST NEWS

Wed, 05 Jun 2024 | 12:06 PM

NIT NA MOI KUINGIA MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA AJALI ZA BARABARANI NCHINI

National Institute of Transport - NIT

Mkuu wa Chuo Dkt. Prosper Mgaya (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI (wa pili kushoto) wakionesha  Mikataba ya ushirikiano kwa waandishi wa habari baada ya kuingia makubaliano ya kushirikiana kutokomeza ajali za Barabarani nchini, tarehe 4 Juni,2024.

Ushirikiano huo utasaidia kwanza kuimarisha eneo la huduma ya kwanza pale ajali inapotokea lakini pia ushirikiano huu utasaidia kupatikana kwa takwimu sahihi za ajali za barabarani kwani majeruhi wengi wa ajali hizi wanatibiwa katika hospital ya MOI.

Latest News

National Institute of Transport - NIT

π—‘π—œπ—§ π—¬π—”π—œπ—•π—¨π—žπ—” π— π—¦π—›π—œπ—‘π——π—œ π—ͺ𝗔 π—žπ—ͺ𝗔𝗑𝗭𝗔 π—žπ—ͺπ—˜π—‘π—¬π—˜ π— π—”π—’π—‘π—˜π—¦π—›π—’ 𝗬𝗔 π—žπ—’π—‘π—šπ—”π— π—”π—‘π—’ π—Ÿπ—” π—§π—œπ—¦π—” π—Ÿπ—” π—ͺπ—”π—›π—”π—‘π——π—œπ—¦π—œ π—ͺ𝗔𝗑𝗔π—ͺπ—”π—žπ—˜ π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” (𝗧𝗔π—ͺπ—˜π—–π—˜)

Aug. 30, 2024, 8:57 a.m.

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeibuka mshindi wa kwanza (1) kati ya Taasisi kumi na moja(11) za Elimu ya Juu ambazo zimeshiriki kwenye maonesho ya kongamano la tisa 9 la wahandisi wanawake Tanzania (Tawece) na kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza.

Kongamano hilo limefanyika jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) kuanzia tarehe 21 hadi 22 Agosti,2024.

Mkuu wa Idara ya π™€π™‘π™šπ™˜π™©π™§π™€π™£π™žπ™˜π™¨ 𝙖𝙣𝙙 π™π™šπ™‘π™šπ™˜π™€π™’π™’π™ͺπ™£π™žπ™˜π™–π™©π™žπ™€π™£ π™€π™£π™œπ™žπ™£π™šπ™šπ™§π™žπ™£π™œ Bi. Grace Kibweja amepokea tuzo hiyo ya mshindi wa kwanza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo.