Thu, 16 Jan 2025 | 10:45 AM
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya uchukuzi ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya wataalam wa Sekta ya Uchukuzi kwa lengo la kuwatambua na kuwasajili wataalam wa Sekta hiyo.
Kauli hiyo imetolewa Desemba 20, 2024 na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile katika mahafali ya 40 ya Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), amesema bodi hiyo pia itakuwa na jukumu la kusimamia weledi na maadili ya watalaam wa Sekta ya Uchukuzi Tanzania Bara.
"Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo NIT, ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Sekta ya Uchukuzi , lengo la Bodi hii litakuwa kuwatambua, kuwasajili na kusimamia weledi na maadili ya wataalam wa Sekta ya Uchukuzi Tanzania Bara,"amesema Kihenzile.
Amesema uanzishwaji wa bodi hiyo una lengo la kuhakikisha kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki.
Akizungumzia kuhusu NIT, Kihenzile amesema Serikali itaendelea kukiwezesha Chuo ili kuhakikisha kinatimiza majukumu yake ya kuandaa wataalam, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam katika sekta ya uchukuzi kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu.
"Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi, inafahamu vizuri mahitaji muhimu ya Chuo, ikiwa ni pamoja na ubora wa miundombinu ya kujifunzia, majengo, ofisi za wahadhiri na mabweni ya wanafunzi. Aidha, natambua kuwa Chuo kipo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa baadhi ya miundombinu hiyo kupitia mradi wa EASTRIP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia(WB) ikiwemo mabweni ambayo nimejulishwa yamekamilika kwa asilimia 97 na majengo ya kituo cha Umahiri ya Usafiri wa Anga ambayo yamekamilika kwa asilimia 90.
"Napenda kuchukua nafasi hii kuuagiza Uongozi wa Chuo kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika kwa kuwa mahitaji ni makubwa vilevile ninauagiza Uongozi kuendelea kutumia mapato ya ndani katika kuendeleza na kuboresha miundombinu ya Chuo,"amesisitiza Kihenzile.
Amesema amefarijika kusikia chuo kimeendelea kutanua wigo wa kutoa mafunzo katika sekta hii muhimu ya Uchukuzi, ikiwa ni pamoja na kujiimarisha katika Njia zote za Usafirishaji yaani Usafiri wa Anga, Maji, Reli, Barabara na Usafiri kwa njia ya mabomba. Mhe. Kihenzile pia amewataka wadau na wafaidika wa shughuli za chuo kwa pamoja na taasisi za umma na binafsi kuunga mkono jitihada za Chuo katika kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni ili ziweze kutumika kwa maendeleo ya nchi.
Awali Mkuu wa Chuo cha NIT, Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya amesema katika mahafali hayo wahitimu 4176 wametunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali kati yao wanaume ni 2,581 na wanawake 1,595.
"Kati ya wahitimu 4176 waliohitimu 29 wametunukiwa shahada ya Uzamili, 6 wametunukiwa statashahada ya uzamili,wahitimu 3,077 wametunukiwa shahada ya kwanza,wahitimu 36 wametunukiwa stashahada ya juu huku wahitimu 909 wametunukiwa stashahada ya kawaida, wahitimu 22 astashahada na wahitimu 22 wakitumikiwa astashahada ya awali,"amesema Dkt.Mgaya.
Akizungumzia changamoto amesema Chuo kimekuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na upungufu wa rasilimali watu sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwakuweka mikakati mbalimbali.
"Ili kukabiliana na upungufu wa miundombinu Chuo kimeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ambapo kwa sasa kinaendelea na ujenzi wa mabweni mawili ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzo 1,500, ujenzi huu unatarajiwa kukamilika Januari 2025,"alisema Dk.Mgaya
Amesema sambamba na mabweni Chuo kinajenga ofisi, madarasa na karakana ambapo jumla ya majengo matatu yanajengwa na yanatarajiwa kukamilika Februari 2025 ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa EASTRIP.
Amesema chuo pia kinaanzisha kampasi mpya mkoani Lindi na Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kampasi ya Dar es Salaam.
Kuhusu rasilimali watu amesema chuo kinaendelea kuomba vibali vya ajira mpya kwa watumishi kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukabiliana na upungufu wa watumishi sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi. Ili kupunguza matumizi ya wahadhiri wa muda (Part-time lecturers).
astashahada na wahitimu 22 wakitumikiwa astashahada ya awali,"amesema Dkt.Mgaya.

50 YEARS NIT ANNIVERSARY 1975-2025
Excellence in Transport for a Sustainable Economy.