Wed, 26 Mar 2025 | 09:57 AM
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia Kituo chake cha Kikanda cha Umahiri katika Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Kasulu Kitengo cha Usalama Barabarani - Dawati la Elimu kimeanza kutoa mafunzo ya siku tano (5) ya usalama barabarani yanayolenga wanafunzi wa shule za msingi, madereva wa bodaboda, bajaji na magari madogo ya abiria wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Akizungumza na waandishi habari baada ya mafunzo hayo yaliyoanza rasmi tarehe 17.3.2025 katika shule za msingi za Murubona, Kalema, Kigamano, Umoja na Kimobwa, Mkuu wa Kituo cha
Kikanda cha Umahiri katika Usalama Barabarani - NIT, Ndg. Godlisten Msumanje amesema lengo la mafunzo hayo ni kuelimisha wanafunzi wa shule za msingi, madereva wa bodaboda, bajaji na magari madogo ya abiria kuhusu matumizi salama na sahihi ya barabara ili kusaidia kupunguza ajali na kuboresha usalama wa watumiaji wa barabara.
Kwa upande wa wanafunzi waliopatiwa mafunzo hayo wamekishukuru Chuo kwa kutoa mafunzo hayo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani kwa kuwaelimisha wenzao.
50 YEARS NIT ANNIVERSARY 1975-2025
Excellence in Transport for a Sustainable Economy.