National Institute of Transport - NIT
Bonyeza Kuthibitisha

ALL NEWS

All News

National Institute of Transport - NIT

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA UKAGUZI WA BARABARA SALAMA KANDA YA KATI -DODOMA

March 16, 2024, 12:25 p.m.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule, amefungua mafunzo ya ukaguzi wa barabara salama kanda ya kati siku ya Jumanne tarehe 05 Machi,2024. Akifungua Mafunzo hayo Mhe.Rosemary Senyamule amesema kila mmoja akipata jambo anahisi yupo peke ake wakulishughulikia kumbe sio hivyo kuwepo kwa wadau mbalimbali kwenye haya mafunzo ni dhahiri kuwa kila mmoja wetu anayo nafasi na tukikaa kwa pamoja tukakubaliana na tukishirikiana basi tutaweza kufika kwenye urahisi wa kuzuia changamoto za ajali zinazotokea na kuleta usalama barabarani kama ilivyo lengo la mafunzo haya kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake Naye Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Zainabu Mshana wakati akitoa hotuba yake alieleza kuwa msukumo wa kutoa mafunzo hayo umetokana na ongezeko la matukio ya vifo yanayotokana na ajali barabarani takwimu inaonesha kuwepo kwa idadi kubwa ya watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa hususa ni vijana umri mdogo ambao ndio nguvu kazi kwa Taifa letu hivyo basi, Chuo kimejipanga kuwajengea uwezo wataalamu wakutoa elimu kwa jamii kama Taifa tuweze kupunguza kabisa ajali za barabarani Tanzania bila ajali inawezekana. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kupitia Mradi wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration (EASTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia umeweza kufanikisha Mafunzo ya Ukaguzi Barabara Salama yanayoendelea kufanyika katika Kanda mbalimbali nchini.

STAND UP, SPEAK OUT, STOP CORRUPTION

Rushwa huzuia Maendeleo, Toa taarifa linda Haki.