National Institute of Transport - NIT

ALL NEWS

All News

National Institute of Transport - NIT

CPA AND CPSP REVIEW CLASSES ADVERTISEMENT

Jan. 21, 2025, 9:54 a.m.

National Institute of Transport - NIT

New Year 2025 Greetings

Jan. 16, 2025, 10:49 a.m.

Dear Esteemed NIT Stakeholders,

As we welcome the New Year, I want to take this opportunity to extend my heartfelt gratitude to each of you for your invaluable contributions  to the National Institute of Transport (NIT). Your support and collaboration  have played a pivotal role in our growth and success, and we are truly  thankful for your commitment to our shared vision and mission.

This year is particularly special as we embark on a journey towards 2025,  when we will proudly celebrate 50 years since the establishment of our  Institute. This milestone is a testament to the strength of our partnerships  and the impact we have made together in the Transport Sector. Together,  we have made significant strides in training, research & innovation, and  consultancy in the Sector.

We are excited about the upcoming 50th anniversary celebrations and the  possibilities that lie ahead. Your continued engagement will be essential as  we honour our past achievements and look forward to an innovative future.

On behalf of the NIT Community, I would like to wish you and your families  a prosperous New Year 2025 that will bring you joy, success and health! Once  again, thank you for being a vital stakeholder of the National Institute of  Transport.

National Institute of Transport - NIT

NIT YASHEHEREKEA MAHAFALI YA 40, BODI YA WATAALAM WA SEKTA YA UCHUKUZI KUUNDWA

Jan. 16, 2025, 10:45 a.m.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya uchukuzi ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya wataalam wa Sekta ya Uchukuzi  kwa lengo la kuwatambua na kuwasajili wataalam wa Sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa Desemba 20, 2024 na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile katika mahafali ya 40 ya Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji  (NIT), amesema bodi hiyo pia itakuwa na jukumu la kusimamia weledi na maadili ya watalaam wa Sekta ya Uchukuzi Tanzania Bara.

"Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo NIT, ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Sekta ya Uchukuzi , lengo la Bodi hii litakuwa kuwatambua, kuwasajili na kusimamia weledi na maadili ya wataalam wa Sekta ya Uchukuzi Tanzania Bara,"amesema Kihenzile.

Amesema uanzishwaji wa bodi hiyo una lengo la kuhakikisha  kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki.

Akizungumzia kuhusu NIT, Kihenzile amesema  Serikali itaendelea kukiwezesha Chuo  ili kuhakikisha  kinatimiza majukumu yake ya kuandaa wataalam, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam katika sekta ya uchukuzi kwa maendeleo  endelevu ya Taifa letu.

"Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi, inafahamu vizuri mahitaji muhimu ya Chuo, ikiwa ni pamoja na ubora wa miundombinu ya kujifunzia, majengo, ofisi za wahadhiri na mabweni ya wanafunzi. Aidha, natambua kuwa Chuo kipo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa baadhi ya miundombinu hiyo kupitia mradi wa EASTRIP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia(WB) ikiwemo mabweni ambayo nimejulishwa yamekamilika kwa asilimia 97 na majengo ya kituo cha Umahiri ya Usafiri wa Anga ambayo yamekamilika kwa asilimia 90.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuuagiza Uongozi wa Chuo kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika kwa kuwa mahitaji ni makubwa vilevile ninauagiza Uongozi kuendelea kutumia mapato ya ndani katika kuendeleza na kuboresha miundombinu ya Chuo,"amesisitiza Kihenzile.

Amesema amefarijika kusikia chuo kimeendelea kutanua wigo wa kutoa mafunzo katika sekta hii muhimu ya Uchukuzi, ikiwa ni pamoja na kujiimarisha katika Njia zote za Usafirishaji yaani Usafiri wa Anga, Maji, Reli, Barabara na Usafiri kwa njia ya mabomba. Mhe. Kihenzile pia amewataka wadau na wafaidika wa shughuli za chuo kwa pamoja na taasisi za umma na binafsi kuunga mkono jitihada za Chuo katika kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni ili ziweze kutumika kwa maendeleo ya nchi.

Awali Mkuu wa Chuo cha NIT, Mhandisi  Dkt. Prosper Mgaya amesema katika mahafali hayo  wahitimu 4176  wametunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali kati yao wanaume  ni 2,581 na wanawake 1,595.

"Kati ya wahitimu 4176 waliohitimu 29 wametunukiwa shahada ya Uzamili, 6 wametunukiwa statashahada ya uzamili,wahitimu 3,077 wametunukiwa shahada ya kwanza,wahitimu 36 wametunukiwa stashahada ya juu huku wahitimu 909 wametunukiwa stashahada ya kawaida, wahitimu 22  astashahada na wahitimu 22 wakitumikiwa astashahada ya awali,"amesema Dkt.Mgaya.

Akizungumzia  changamoto amesema Chuo kimekuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali  ikiwemo miundombinu na upungufu wa rasilimali watu sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwakuweka mikakati mbalimbali.

"Ili kukabiliana na upungufu wa miundombinu Chuo kimeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ambapo kwa sasa kinaendelea na ujenzi wa mabweni mawili ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzo 1,500, ujenzi huu unatarajiwa kukamilika Januari 2025,"alisema Dk.Mgaya

Amesema sambamba na mabweni Chuo kinajenga ofisi, madarasa na karakana ambapo jumla ya majengo matatu yanajengwa na yanatarajiwa kukamilika Februari 2025 ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa EASTRIP.

Amesema chuo pia kinaanzisha kampasi mpya mkoani Lindi na Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kampasi ya Dar es Salaam.

Kuhusu rasilimali watu amesema chuo kinaendelea kuomba vibali vya ajira mpya kwa watumishi kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukabiliana na upungufu wa watumishi sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi. Ili kupunguza matumizi ya wahadhiri wa muda (Part-time lecturers).

astashahada na wahitimu 22 wakitumikiwa astashahada ya awali,"amesema Dkt.Mgaya.

Akizungumzia  changamoto amesema Chuo kimekuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali  ikiwemo miundombinu na upungufu wa rasilimali watu sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwakuweka mikakati mbalimbali.

"Ili kukabiliana na upungufu wa miundombinu Chuo kimeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ambapo kwa sasa kinaendelea na ujenzi wa mabweni mawili ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzo 1,500, ujenzi huu unatarajiwa kukamilika Januari 2025,"alisema Dk.Mgaya

Amesema sambamba na mabweni Chuo kinajenga ofisi, madarasa na karakana ambapo jumla ya majengo matatu yanajengwa na yanatarajiwa kukamilika Februari 2025 ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa EASTRIP.

Amesema chuo pia kinaanzisha kampasi mpya mkoani Lindi na Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kampasi ya Dar es Salaam.

Kuhusu rasilimali watu amesema chuo kinaendelea kuomba vibali vya ajira mpya kwa watumishi kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukabiliana na upungufu wa watumishi sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi. Ili kupunguza matumizi ya wahadhiri wa muda (Part-time lecturers).

 

TIME TABLE FOR DISBURSE OF GRADUATION GOWNS FROM 07TH DECEMBER, 2024

Dec. 6, 2024, 3:57 p.m.

INVITATION TO ATTEND 11th CONVOCATION AND 40th GRADUATION CEREMONIES

Dec. 3, 2024, 1:57 p.m.

LIST OF GRADUANDS FOR ACADEMIC YEAR 2023/2024

Dec. 2, 2024, 10:35 a.m.

National Institute of Transport - NIT

KUWASILISHA MAOMBI YA KUISHIΒ  KATIKA HOSTELI ZA CHUO

Oct. 4, 2024, 10:48 a.m.

 

 

 

KWA KUWASILISHA MAOMBI YA KUISHI  KATIKA HOSTELI ZA CHUO 

BONYEZA HAPA https://sims.nit.ac.tz/

 

KOZI YA WATOA HUDUMA KWENYE MABASI

Sept. 13, 2024, 3:35 p.m.

National Institute of Transport - NIT

ππˆπ“ π˜π€π“πŽπ€ πŒπ€π…π”ππ™πŽ π˜π€ π”π’π€π‹π€πŒπ€ ππ€π‘π€ππ€π‘π€ππˆ πŠπ–π€ πŒπ€πƒπ„π‘π„π•π€ 𝐍𝐀 πŒπ€πŠπŽππƒπ€πŠπ“π€ πŒπŠπŽπ€ 𝐖𝐀 πŠπ”π’πˆππˆ 𝐔𝐍𝐆𝐔𝐉𝐀

Aug. 30, 2024, 9:04 a.m.

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia Kituo chake cha Kikanda cha Umahiri katika Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar (ZARTSA) kimetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva na makondakta wa gari za abiria wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku moja (1) yaliyofanyika tarehe 21.11.2024 Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yale yote watakayojifunza ili kuondoa changamoto ya ajali za barabarani Zanzibar ambazo zimesababisha vifo na ulemavu kwa watu wengi.

Pia Mhe. Mahmoud ameushukuru Uongozi wa Chuo kwa kutoà mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva na makondakta wa magari ya abiria katika Mkoa wa Kusini Unguja.

Naye Mkuu wa Kituo cha
Kikanda cha Umahiri katika Usalama Barabarani - NIT, Ndg. Godlisten Msumanje amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo madereva na makondakta juu ya matumizi sahihi ya barabara.

Kwa upande wa madereva na makonda waliyopatiwa mafunzo hayo wamekishukuru Chuo kwa kutoa mafunzo hayo na kuahidi kuzingatia yale yote waliojifunza ili kuboresha utendaji wa kazi zao.

National Institute of Transport - NIT

NIT YATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA SHULE ZA MSINGI KUMI NA MOJA (11)

Aug. 30, 2024, 9:01 a.m.

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia kituo chake cha Umahiri cha Kikanda Katika Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Elimu ya Usalama Barabarani kimetoa Mafunzo ya Usalama Barabarani Mkoani Dodoma.

Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 28.8.2024 na 29.8.2024 wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kumi na moja(11) ikiwemo shule ya msingi Mazengo ,Kikuyu,Amani,Mlezi, Mlimani, Makole, Kizota, Chadulu, Mlimwa, na Kisasa.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea wanafunzi hao uwelewa wa matumizi sahihi ya barabara.