Jan. 16, 2025, 10:45 a.m.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya uchukuzi ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya wataalam wa Sekta ya Uchukuzi kwa lengo la kuwatambua na kuwasajili wataalam wa Sekta hiyo.
Kauli hiyo imetolewa Desemba 20, 2024 na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile katika mahafali ya 40 ya Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), amesema bodi hiyo pia itakuwa na jukumu la kusimamia weledi na maadili ya watalaam wa Sekta ya Uchukuzi Tanzania Bara.
"Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo NIT, ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Sekta ya Uchukuzi , lengo la Bodi hii litakuwa kuwatambua, kuwasajili na kusimamia weledi na maadili ya wataalam wa Sekta ya Uchukuzi Tanzania Bara,"amesema Kihenzile.
Amesema uanzishwaji wa bodi hiyo una lengo la kuhakikisha kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki.
Akizungumzia kuhusu NIT, Kihenzile amesema Serikali itaendelea kukiwezesha Chuo ili kuhakikisha kinatimiza majukumu yake ya kuandaa wataalam, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam katika sekta ya uchukuzi kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu.
"Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi, inafahamu vizuri mahitaji muhimu ya Chuo, ikiwa ni pamoja na ubora wa miundombinu ya kujifunzia, majengo, ofisi za wahadhiri na mabweni ya wanafunzi. Aidha, natambua kuwa Chuo kipo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa baadhi ya miundombinu hiyo kupitia mradi wa EASTRIP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia(WB) ikiwemo mabweni ambayo nimejulishwa yamekamilika kwa asilimia 97 na majengo ya kituo cha Umahiri ya Usafiri wa Anga ambayo yamekamilika kwa asilimia 90.
"Napenda kuchukua nafasi hii kuuagiza Uongozi wa Chuo kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika kwa kuwa mahitaji ni makubwa vilevile ninauagiza Uongozi kuendelea kutumia mapato ya ndani katika kuendeleza na kuboresha miundombinu ya Chuo,"amesisitiza Kihenzile.
Amesema amefarijika kusikia chuo kimeendelea kutanua wigo wa kutoa mafunzo katika sekta hii muhimu ya Uchukuzi, ikiwa ni pamoja na kujiimarisha katika Njia zote za Usafirishaji yaani Usafiri wa Anga, Maji, Reli, Barabara na Usafiri kwa njia ya mabomba. Mhe. Kihenzile pia amewataka wadau na wafaidika wa shughuli za chuo kwa pamoja na taasisi za umma na binafsi kuunga mkono jitihada za Chuo katika kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni ili ziweze kutumika kwa maendeleo ya nchi.
Awali Mkuu wa Chuo cha NIT, Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya amesema katika mahafali hayo wahitimu 4176 wametunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali kati yao wanaume ni 2,581 na wanawake 1,595.
"Kati ya wahitimu 4176 waliohitimu 29 wametunukiwa shahada ya Uzamili, 6 wametunukiwa statashahada ya uzamili,wahitimu 3,077 wametunukiwa shahada ya kwanza,wahitimu 36 wametunukiwa stashahada ya juu huku wahitimu 909 wametunukiwa stashahada ya kawaida, wahitimu 22 astashahada na wahitimu 22 wakitumikiwa astashahada ya awali,"amesema Dkt.Mgaya.
Akizungumzia changamoto amesema Chuo kimekuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na upungufu wa rasilimali watu sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwakuweka mikakati mbalimbali.
"Ili kukabiliana na upungufu wa miundombinu Chuo kimeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ambapo kwa sasa kinaendelea na ujenzi wa mabweni mawili ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzo 1,500, ujenzi huu unatarajiwa kukamilika Januari 2025,"alisema Dk.Mgaya
Amesema sambamba na mabweni Chuo kinajenga ofisi, madarasa na karakana ambapo jumla ya majengo matatu yanajengwa na yanatarajiwa kukamilika Februari 2025 ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa EASTRIP.
Amesema chuo pia kinaanzisha kampasi mpya mkoani Lindi na Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kampasi ya Dar es Salaam.
Kuhusu rasilimali watu amesema chuo kinaendelea kuomba vibali vya ajira mpya kwa watumishi kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukabiliana na upungufu wa watumishi sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi. Ili kupunguza matumizi ya wahadhiri wa muda (Part-time lecturers).
astashahada na wahitimu 22 wakitumikiwa astashahada ya awali,"amesema Dkt.Mgaya.
Akizungumzia changamoto amesema Chuo kimekuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na upungufu wa rasilimali watu sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwakuweka mikakati mbalimbali.
"Ili kukabiliana na upungufu wa miundombinu Chuo kimeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ambapo kwa sasa kinaendelea na ujenzi wa mabweni mawili ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzo 1,500, ujenzi huu unatarajiwa kukamilika Januari 2025,"alisema Dk.Mgaya
Amesema sambamba na mabweni Chuo kinajenga ofisi, madarasa na karakana ambapo jumla ya majengo matatu yanajengwa na yanatarajiwa kukamilika Februari 2025 ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa EASTRIP.
Amesema chuo pia kinaanzisha kampasi mpya mkoani Lindi na Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kampasi ya Dar es Salaam.
Kuhusu rasilimali watu amesema chuo kinaendelea kuomba vibali vya ajira mpya kwa watumishi kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukabiliana na upungufu wa watumishi sambamba na ongezeko la udahili wa wanafunzi. Ili kupunguza matumizi ya wahadhiri wa muda (Part-time lecturers).
Sept. 13, 2024, 3:35 p.m.
Aug. 30, 2024, 9:04 a.m.
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia Kituo chake cha Kikanda cha Umahiri katika Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar (ZARTSA) kimetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva na makondakta wa gari za abiria wa Mkoa wa Kusini Unguja.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku moja (1) yaliyofanyika tarehe 21.11.2024 Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yale yote watakayojifunza ili kuondoa changamoto ya ajali za barabarani Zanzibar ambazo zimesababisha vifo na ulemavu kwa watu wengi.
Pia Mhe. Mahmoud ameushukuru Uongozi wa Chuo kwa kutoà mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva na makondakta wa magari ya abiria katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Naye Mkuu wa Kituo cha
Kikanda cha Umahiri katika Usalama Barabarani - NIT, Ndg. Godlisten Msumanje amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo madereva na makondakta juu ya matumizi sahihi ya barabara.
Kwa upande wa madereva na makonda waliyopatiwa mafunzo hayo wamekishukuru Chuo kwa kutoa mafunzo hayo na kuahidi kuzingatia yale yote waliojifunza ili kuboresha utendaji wa kazi zao.
Aug. 30, 2024, 9:01 a.m.
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia kituo chake cha Umahiri cha Kikanda Katika Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Elimu ya Usalama Barabarani kimetoa Mafunzo ya Usalama Barabarani Mkoani Dodoma.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 28.8.2024 na 29.8.2024 wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kumi na moja(11) ikiwemo shule ya msingi Mazengo ,Kikuyu,Amani,Mlezi, Mlimani, Makole, Kizota, Chadulu, Mlimwa, na Kisasa.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea wanafunzi hao uwelewa wa matumizi sahihi ya barabara.
Aug. 30, 2024, 8:59 a.m.
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia kituo chake cha Umahiri cha Kikanda katika Usalama Barabarani (Regional Centre of Excellence for Road Safety) imetoa Mafunzo ya Udereva wa Magari ya Mizigo (HGV) kwa madereva kumi na nne (14).
Mafunzo hayo yameanza tarehe 19.08.2024 na yanatarajia kumalizika tarehe 31.08.2024 katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Mkoani Dodoma
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na umahiri madereva hao katika kuendesha magari ya mizigo kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.
Aug. 30, 2024, 8:57 a.m.
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeibuka mshindi wa kwanza (1) kati ya Taasisi kumi na moja(11) za Elimu ya Juu ambazo zimeshiriki kwenye maonesho ya kongamano la tisa 9 la wahandisi wanawake Tanzania (Tawece) na kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza.
Kongamano hilo limefanyika jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) kuanzia tarehe 21 hadi 22 Agosti,2024.
Mkuu wa Idara ya ππ‘πππ©π§π€π£πππ¨ ππ£π πππ‘πππ€π’π’πͺπ£ππππ©ππ€π£ ππ£πππ£πππ§ππ£π Bi. Grace Kibweja amepokea tuzo hiyo ya mshindi wa kwanza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo.
June 8, 2024, 10:41 p.m.
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji chaendelea kutoa mafunzo kwa Wahudumu wa Mabasi ya Masafa Marefu na Mijini - Dar es salaam. Mafunzo hayo ya siku sita (6) yalianza siku ya Jumatatu tarehe 03.06.2024 na kuhitimishwa siku ya Jumamosi tarehe 08.06.2024 ambapo jumla ya washiriki 43 wemehudhuria mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti.
Akizungumza na washiriki wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo hayo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Kituo cha Ukaguzi wa Magari uliyopo katika kampasi ya Chuo Mabibo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Dkt. John Mahona
amewaasa washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yale yote
waliyojifunza ili kuleta tija na mabadiliko chanya katika vituo vyao vya kazi. Amesema
"Mkayazingatie yote mliyofundishwa ili kuleta tija katika vituo vyenu vya kazi"
June 8, 2024, 10:36 p.m.
NIT students participated in a one-day workshop organized by the Carter Center in collaboration with China-Africa Vocational Education Cooperation Alliance (CAVECA).
The workshop was held at NIT main campus Mabibo Dar es Salaam on Saturday 8th June 2024 focusing on empowering students with knowledge on the importance of climate - resilient infrastructure such as flood plains, embankments and other systems to reduce vulnerability to climate -related hazards such as floods and landslides.
June 5, 2024, 12:08 p.m.
Mkuu wa Chuo Dkt. Prosper Mgaya (kushoto) akikabidhia vitabu na Meneja wa Kampuni ya Simba Supply Chain Solutions Ndg. Ajuaye Kheri Msese vinavyoelimisha umuhimu wa kubadili tabia kwa watumiaji wa Barabara "Mfumo Mahiri wa Msingi wa Kitabia" mara baada ya kuhuisha Mkataba wa Ushirikiano baina yaTaasisi hizo mbili, tarehe 4 Juni, 2024.
June 5, 2024, 12:06 p.m.
Mkuu wa Chuo Dkt. Prosper Mgaya (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI (wa pili kushoto) wakionesha Mikataba ya ushirikiano kwa waandishi wa habari baada ya kuingia makubaliano ya kushirikiana kutokomeza ajali za Barabarani nchini, tarehe 4 Juni,2024.
Ushirikiano huo utasaidia kwanza kuimarisha eneo la huduma ya kwanza pale ajali inapotokea lakini pia ushirikiano huu utasaidia kupatikana kwa takwimu sahihi za ajali za barabarani kwani majeruhi wengi wa ajali hizi wanatibiwa katika hospital ya MOI.
50 YEARS NIT ANNIVERSARY 1975-2025
"Excellence in Transport for Sustainable Economy"