National Institute of Transport - NIT
Bonyeza Kuthibitisha

ALL NEWS

All News

DRIVING SHORT COURSES ACTION PROGRAMME FROM JANUARY – JUNE, 2024.

April 16, 2024, 9:40 p.m.

National Institute of Transport - NIT

MKUU WA CHUO AFANYA ZIARA KUTEMBELEA MIRADI YA CHUO

March 16, 2024, 12:28 p.m.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Dkt. Prosper Mgaya leo tarehe 15.3.2024,amefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya ujenzi ambayo Chuo inaendelea kutekelezwa katika kampasi ya Chuo Mabibo jijini Dar es salaam. Dkt. Mgaya ametembelea miradi kadhaa ikiwemo mradi wa ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi, ujenzi wa jengo la kituo cha umahiri cha mafunzo ya anga na operesheni za usafirishaji, ujenzi wa jengo la mafunzo ya wahudumu wa ndani ya ndege, ujenzi wa maabara ya kisasa, ujenzi wa uzio wa Chuo na ukarabati wa maktaba ya Chuo. Akizungumza wakati wa ziara hiyo Dkt. Mgaya amewasisitiza wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa majengo hayo kwa wakati ambao pande mbili zimekubaliana.

National Institute of Transport - NIT

DKT. PROSPER MGAYA AWASILI RASMI CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI

March 16, 2024, 12:27 p.m.

Dkt. Prosper Mgaya amewasili rasmi Chuoni leo tarehe 14 Machi,2024 na kukutana na Menejimenti ya Chuo. Akizungumza na Menejimenti ya Chuo Dkt.Mgaya amesisitiza dhamira yake ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwa weledi na ubunifu ili kutimiza malengo ya Chuo. ‘’NIT ni Chuo cha kisekta, hivyo jamii na Serikali ina matarajio makubwa na Chuo chetu kwahiyo tuna kazi kubwa ya kufanya ili kukidhi matarajio hayo …. Tujipange wote kwa pamoja ili tuweze kusonga mbele na uwezo wa kufanya hivyo tunao”. Dkt. Mgaya amesema kuwa kazi ya kiongozi ni kutambua na kutumia uwezo wa watu alionao na kuendelea kurekebisha mapungufu yao, hivyo amewataka Viongozi wa Chuo kuwatazama watumishi wao katika muktadha huo ili kufanikisha malengo ya Chuo. Amewasihi Viongozi kufanya kazi kwa ushirikiano na kutambua mchango wa kila mmoja kwasababu hakuna anayeweza kufanikisha malengo ya Taasisi akiwa peke yake. Amesisitiza kila mmoja afanye kazi yake kwa uadilifu na juhudi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 4 Machi 2024 alimteua Dkt. Mgaya kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Dkt. Mgaya anachukua nafasi ya Prof.Zacharia Mganilwa ambaye alimaliza muda wake wa utumishi wa umma mwezi Novemba, 2023, na nafasi hiyo kukaimiwa na Dkt. Zainabu Mshana ambaye ni Naibu Mkuu wa Chuo – Mipango Fedha na Utawala, kabla ya uteuzi huo Dkt. Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA

National Institute of Transport - NIT

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI - KIGAMBONI

March 16, 2024, 12:26 p.m.

NIT katika Sherehe kuadhimisha ya Siku ya wanawake duniani, Mjimwema Kigamboni.

National Institute of Transport - NIT

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA UKAGUZI WA BARABARA SALAMA KANDA YA KATI -DODOMA

March 16, 2024, 12:25 p.m.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule, amefungua mafunzo ya ukaguzi wa barabara salama kanda ya kati siku ya Jumanne tarehe 05 Machi,2024. Akifungua Mafunzo hayo Mhe.Rosemary Senyamule amesema kila mmoja akipata jambo anahisi yupo peke ake wakulishughulikia kumbe sio hivyo kuwepo kwa wadau mbalimbali kwenye haya mafunzo ni dhahiri kuwa kila mmoja wetu anayo nafasi na tukikaa kwa pamoja tukakubaliana na tukishirikiana basi tutaweza kufika kwenye urahisi wa kuzuia changamoto za ajali zinazotokea na kuleta usalama barabarani kama ilivyo lengo la mafunzo haya kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake Naye Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Zainabu Mshana wakati akitoa hotuba yake alieleza kuwa msukumo wa kutoa mafunzo hayo umetokana na ongezeko la matukio ya vifo yanayotokana na ajali barabarani takwimu inaonesha kuwepo kwa idadi kubwa ya watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa hususa ni vijana umri mdogo ambao ndio nguvu kazi kwa Taifa letu hivyo basi, Chuo kimejipanga kuwajengea uwezo wataalamu wakutoa elimu kwa jamii kama Taifa tuweze kupunguza kabisa ajali za barabarani Tanzania bila ajali inawezekana. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kupitia Mradi wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration (EASTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia umeweza kufanikisha Mafunzo ya Ukaguzi Barabara Salama yanayoendelea kufanyika katika Kanda mbalimbali nchini.